Dk. Mpango ahani msiba wa RAS Kilimanjaro

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema watumishi wa Umma wanapaswa kumuenzi aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro marehemu Tixon Nzunda kwa kuwa waadilifu, wazalendo na kumtanguliza Mungu katika majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Makamu wa Rais amesema hayo leo Jumatano wakati akizungumza na waombolezaji alipowasili nyumbani kwa aliyekuwa…

Read More

Uyoga unavyosaidia kuimarisha mishipa ya fahamu

Dar es Salam. Uyoga  ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba na protini ambayo hufanya vizuri katika mwilini wa binadamu. Kama ulikuwa hufahamu uyoga una nyuzi nyuzi nyingi na hauna mafuta  na chumvi ya sodium. Mtaalamu wa Sayansi na Teknolojia ya Chakula, Francis Modaha, anasema uyoga una kundi la vitamini B kwa wingi, yaani vitamini B2  (Riboflavin), Niacin na Pantothenic acid. Anasema…

Read More

Kipa wa JKT Tanzania aitaja penalti ya Simba

KIPA wa JKT Tanzania,  Yakubu Suleiman amesema tangu msimu uanze mechi iliyosalia katika kumbukumbu zake ni dhidi ya Simba, iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex, Desemba 24, 2024. Aliitaja sababu ya kutoisahau  mechi hiyo ambayo ni kufungwa dakika za nyongeza bao la penalti na Jean Ahoua wakati dakika 90 za mchezo akiwa ameokoa hatari nyingi akiamini…

Read More

Serikali mbioni kutangaza ajira 45,000

Dodoma. Serikali imesema kabla ya mwaka huu wa fedha kuisha itakuwa imetangaza nafasi za ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unafanyika. Mwaka wa fedha wa Serikali unakwisha Juni 30 ya kila mwaka, hivyo kwa kauli hiyo, kuna nafasi za ajira zitakazotolewa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa. Kauli hiyo imetolewa bungeni leo…

Read More

Bocco atambulishwa rasmi kuwa mshambuliaji wa JKT Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Simba, John Bocco, ametambulishwa rasmi kuwa mshambuliaji mpya wa klabu ya JKT Tanzania. Bocco, ambaye ni kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya Tanzania, tayari ameanza mazoezi na klabu yake mpya, akijiandaa kwa msimu ujao. Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Bocco kutokana na kutopata nafasi…

Read More

Wanne wajitosa Urais TOC, yumo Mtaka

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ni miongoni mwa wagombea wanne waliojitosa kuwania urais kwenye uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC). Wengine ni makamu wa rais wa TOC anayemaliza muda wake, Henry Tandau, Nasra Juma Mohammed na Michael Washa. Mmoja wa viongozi wa Kamisheni ya uchaguzi huo, ameiambia Mwananchi kwamba wagombea hao watatu…

Read More

Haya hapa yanayomsubiri Dk Migiro ofisi ya Katibu Mkuu

Dodoma/Dar. Wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikimtangaza Balozi Dk Asha-Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wake mpya, wadau mbalimbali wametaja majukumu makubwa yanayomsubiri kiongozi huyo, likiwamo la kuirejesha imani ya chama hicho kwa wanachama na wananchi wasio wanachama. Miongoni mwa mambo yanayobainishwa kama kibarua kikubwa kwa Dk Migiro ni namna ya kwenda sambamba na kasi ya…

Read More