Malindi yarejea Unguja na pointi tatu za Chipukizi
TIMU ya Malindi kutoka Unguja, imefanikiwa kuvuna alama tatu kwa kuifunga Chipukizi bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyochezwa Septemba 27, 2025 kwenye Uwanja Gombani uliopo kisiwani Pemba. Bao hilo lilifungwa na Tchakei Moucheri dakika 15 akimalizia pasi ya Ramadhan Mponda ambapo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa…