WIZARA YA FEDHA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU MZUMBE KUIMARISHA USIMAMIZI WA MALI ZA SERIKALI.
Na. Saidina Msangi, WF, Dodoma. Wizara ya Fedha, imeahidi kuendelea kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe (MU) katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujengeana uwezo katika masuala ya ununuzi, ugavi na usimamizi wa mali za Serikali ili kuandaa wahitimu waliobobea katika sekta hizo. Hayo yalibainishwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bw. Lusius…