Asia Masimba anayewaongoza wanawake 400 wachimbaji madini
Geita. Ujasiri na uthubutu wa Asia Masimba ni simulizi ya kuvunja miiko iliyodumu kwa miongo kadhaa katika sekta ya madini mkoani Geita. Katika mazingira ambayo wanawake walionekana kuwa mkosi machimboni, Asia alithubutu kuingia duarani, akakubali kutukanwa, kufukuzwa na hata kucharazwa viboko, lakini hakurudi nyuma. Kwa miaka mitano mfululizo alipambana na imani potofu zilizotamalaki katika jamii…