Simulizi ya mjane aliyetupiwa vitu nje Mikocheni
Dar es Salaam. “Kama shida ilikuwa hela, angesema marehemu mume wangu hakumlipa mimi ningejua namlipaje, lakini si kudai nyumba ni yake.” Ni kauli ya Alice Haule, mjane aliyefukuzwa kwenye nyumba anayodai ni yake iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam, huku vitu vikitolewa nje. Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala,…