
Yanga kuzindua ‘Tunapiga kichwani’ kesho Dar
Yanga itazindua tamasha la Wiki ya Mwananchi kesho katika Viwanja vya Zakhem vilivyopo Mbagala jijini Dar es Salaam huku ikithibitisha kuwa baadhi ya tiketi zimeisha. Meneja wa Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema katika uzinduzi huo watataja majina ya wasanii watakaonogesha kilele Cha tamasha hilo litakalofanyika Septemba 12. Kamwe amesema wamefanya maboresho makubwa kuelekea kilele…