Mikakati ya Arusha kuwasafisha ombaomba ndani ya miezi sita
Arusha. Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na wataalamu wa maendeleo ya jamii imeweka malengo ya kuwafuta ombaomba wote ndani ya Jiji la Arusha ndani ya miezi sita. Hatua hii inalenga kupunguza kero kwa watalii, wageni na wafanyabiashara jijini humo. Azimio hilo lilifikiwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo…