Mashabiki waiponza Black Sailors, yapigwa faini Sh1 milioni
BODI ya Ligi Zanzibar, imeitoza faini ya Sh1 milioni Black Sailors inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Zanzibar kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo kufanya vurugu baada ya kumalizika kwa mechi. Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichofanyika Desemba 3, 2025, ilipopitia mwenendo na matukio…