Dk Nchimbi atembelea kaburi la hayati Magufuli Chato, aeleza namna ya kumuenzi
Chato. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amesema hakuna namna bora ya kumuenzi Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli zaidi ya kuendeleza kazi aliyoianzisha. Dk Nchimbi ameeleza hayo leo Jumapili, Agosti 11, 2024 baada ya kuwasili Wilaya ya Chato mkoani Geita akitokea Kagera, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake…