MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI: Kipunguni wabuni mbinu kuwashughulikia wanaokatili watoto
Na Nora Damian, Mtanzania Digital Sauti nyingi zinapazwa kila uchao kuhusu ustawi wa watoto kutokana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuripotiwa sehemu mbalimbali nchini ambavyo vingi vinaumiza na kufifisha kizazi kinachotarajiwa kuwa cha kesho. Ripoti ya takwimu za Uhalifu na Usalama Barabarani ya kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2023 iliyotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania…