Simba ni mchaka mchaka, hakuna kulala!

KIKOSI cha Simba kinarudi tena katika kambi ya mazoezi kuanzia leo Jumatatu, ikiwa ni saa chache tangu irejee kutoka kambini jijini Cairo, Misri ilikokuwa kwa muda wa mwezi mmoja ikijifua na kucheza mechi nne za kirafiki za kimataifa za kujipima nguvu. Simba ilianza kambi ya muda mfupi jijini Dar es Salaam kisha Julai 30 ikasafiri…

Read More

Ile ishu ya uwanja Yanga, kazi inaanza upya

KAMA ulidhani Yanga inapiga porojo katika ujenzi wa Uwanja pale Jangwani, tulia kwanza, kwani kuna mambo mazito yameshaanza na habari mpya ni rasmi mchakato wa kuongezewa eneo unakamilika leo Septemba Mosi. Kuanzia kesho Jumanne (Septemba 2), Yanga itakuwa inamiliki eneo la mita za mraba 37,500 pale Jangwani ikiwa ni baada ya kukamilisha eneo ambalo waliliomba…

Read More

CUF yataja mwarobaini wa wizi mali za umma

Mwanza. Chama cha Wananchi (CUF) kimefungua rasmi kampeni zake za kuomba kura kwa wananchi kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu, huku kikisema, wezi wote wa mali za umma hawatafungwa jela isipokiwa watatakiwa kurejesha mali. ‎Ufunguzi huo umefanyika leo Jumapili Agosti 31, 2025 katika Uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza ukihudhuriwa na mwenyekiti…

Read More

Vodacom Tanzania na Don Bosco wazindua mpango wa kuwainua vijana na kuendeleza mpira wa kikapu nchini.

 Vodacom Tanzania PLC imesaini ushirikiano na Shirika la Salesian of Don Bosco Kanda ya Tanzania na kuzindua mfululizo wa mipango inayolenga kuwawezesha vijana na kuendeleza mchezo wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam. Ushirikiano huu umehalalishwa kupitia kusainiwa kwa Makubaliano ya Ushirikiano (MoU), yakionyesha udhamini rasmi wa Vodacom kwa Don Bosco na Ligi ya…

Read More

Simba yajivunia jezi mpya, Mangungu akiweka angalizo

WAKATI Simba ikitamba kuwa jezi zao mpya zinazozinduliwa leo Agosti 31, 2025 zitakuwa za ubora wa hali ya juu, mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amewataka mashabiki na wanachama kuilinda chapa yao. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo unaofanyika leo katika Ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar, Mangungu amesema kuwa jezi zao ni…

Read More

Mgombea urais NLD alia na usawa, heshima

Dar es Salaam. Wakati Chama cha National League for Democracy (NLD) kikiwa kimetangaza kuzindua kampeni zake Septemba 4, 2025 mkoani Tanga, mgombea urais wa chama hicho, Doyo Hassan Doyo, ametoa tahadhari akidai kwamba kwa siku tatu tangu kuanza kwa kampeni, kuna viashiria vya kutokuwepo kwa usawa na heshima kwa wagombea urais. Akizungumza leo Jumapili, Agosti…

Read More