Fyatu kujifyatua na kujinoma na king’ora!
Baada ya kuchoka msongamano wa Bongo isiyo na bongo za kutatua changamoto na kero zake, nimechemsha bongo. Niwajuze waziwazi. Nina mpango wa kununua na kufunga king’ora kwenye mchuma wangu kuepuka kusota kwenye foleni kama mafyatu makapuku wakati mie ni munene wao kama wale wanene wa kaya. Maana, kama sikosei, ndiyo mfumo wa kifyatu wa wanene…