BARAZA LA USHAURI KWA WATU WENYE ULEMAVU LAPONGEZWA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Mary Maganga amelipongeza Baraza la Ushauri la Taifa kwa Watu wenye Ulemavu kwa mchango mkubwa walioutoa katika kuimarisha haki na ustawi kwa Watu Wenye Ulemavu nchini. Amesema juhudi hizo zimekuwa chachu ya mafanikio katika kuendeleza ajenda ya usawa, ushirikishwaji na ulinzi…