Saa 18 za mateso wagonjwa kukosa umeme Muhimbili
Dar es Salaam. Zaidi ya wagonjwa 200 wanaohitaji huduma ya kuchuja damu ‘dialysis’ na watoto wanaopokea huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jana walipitia wakati mgumu baada ya jengo wanalolitumia kupata huduma hizo kukosa umeme kwa saa 18. Wagonjwa hao wanaopokea huduma katika jengo la watoto kwa zamu ndani ya hospitali hiyo, walijikuta wakirundikana…