Mgombea urais wa CUF ashindwa kufika Musoma, ubovu wa barabara watajwa
Musoma. Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Gombo na mgombea mwenza wake, Husna Abdallah wameshindwa kufika katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliopangwa kufanyika mjini Musoma kutokana na changamoto za barabara. Kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), mgombea huyo alitarajiwa kufanya mkutano huo leo, Agosti 2, 2025,…