Rais Samia aagiza kitafutwe kiini cha tatizo, wadau watoa ya moyoni
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameipa jukumu Tume huru ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, kusaka kiini cha tatizo hilo na kuja na mapendekezo yatakayoweka msingi wa maridhiano. Wakati Rais Samia akitoa maelekezo hayo, baadhi ya wadau wameonyesha wasiwasi…