Waamua kuondokana na adha ya kutembea kilomita 15 kufuata huduma za afya, Serikali yawaunga mkono
Tabora. Wananchi wa vijiji vitatu vilivyopo katika Kata ya Ugalla tarafa ya Ussoke Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora, wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 15 kufuata huduma za afya ambapo ni zaidi ya miaka 20 wanaishi katika adha hiyo. Wamebainisha adha hiyo leo Septemba 17, 2025 ambapo wameanzisha ujenzi wa kituo cha afya…