Serikali haina deni MSD, fikisheni huduma kwa wananchi – RAS
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikiendelea kuongeza bajeti ya ununuzi wa bidhaa za afya, Bohari ya Dawa (MSD) na watumishi katika sekta ya famasia wameagizwa kusimamia kwa usahihi mnyororo wa ugavi wa bidhaa hizo, ili kuleta tija kwa wananchi ikiwamo kupata huduma bora bila manung’uniko. Hayo yamesemwa leo Jumatano, Septemba 17, 2025 na Katibu Tawala…