Huko Yanga kuna fukuta, kocha aitwa mezani
YANGA ilirejea nyumbani jana kwa mafungu ikitokea Mkoani Dodoma ilikokwenda kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kutengeneza sare nyingine ya tano msimu huu lakini matokeo hayo yameibua presha kubwa kwa kocha wa timu hiyo Pedro Goncalves. Presha kubwa ya Pedro ni kwamba Yanga ikiwa chini yake haijapoteza mchezo wowote lakini kwenye sare…