Wanaodaiwa kuiibia benki Sh5.7 bilioni bado wanajadiliana na DPP
Dar es Salaam. Upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili washtakiwa tisa wanaodaiwa kuongoza genge la uhalifu na kujipatia zaidi ya Sh5.7 bilioni kwa udanganyifu mali ya Equity Bank Tanzania Limited, umedai bado unaendelea na majadiliano ya kumaliza kesi hiyo. Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, wizi na…