Uchaguzi Mkuu 2025: Musukuma alipuka bungeni
Dodoma. Homa ya uchaguzi imeendelea kutanda bungeni ambapo Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma ameshauri watumishi wa umma wanaotaka kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, wafanyiwe ukaguzi maalumu ili kuepuka Bunge kuwa sehemu ya vichaka vya kujificha watu wasio waadilifu. Musukuma ametoa angalizo hilo kipindi ambacho vuguvugu la uchaguzi katika majimbo limepamba…