
WATALAAMU WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WIZARA YA MALIASILI WAHIMIZWA KUWA KIDIGITALI
…………….. Na Sixmund Begashe, Dodoma Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuzingatia matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi katika uchakataji, uhifadhi na upatikanaji wa taarifa kwa wakati. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara…