
Bado Watatu – 11 | Mwanaspoti
“AFANDE kama ulivyosema alama za dole gumba ni zile zile za kwanza. Hii imethibitisha kwamba muuaji ni mtu yule yule,” Ibrahim akaniambia kabla sijakaa kwenye kiti. Nilipokaa nikamuuliza: “Na zile alama za marehemu mmeshazichunguza?” “Tumezichunguza kujua kama ni mtu ambaye tuna rekodi naye lakini tumepata matokeo ya kushangaza kama yale tuliyoyapata mwanzo ndio maana nimekuita.”…