
Chadema kugharamia elimu watoto wa marehemu Nyalusi
Iringa. Katika hatua inayoonyesha mshikamano wa kijamii na kisiasa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeamua kugharamia masomo ya watoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Iringa Mjini, marehemu Frank Nyalusi. Akizungumza leo Jumatatu, Septemba 22, 2025, katika ofisi za chama hicho zilizopo Veta Manispaa ya Iringa, Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti, Jackson…