Simulizi binti alivyochomwa moto kwa tuhuma za wizi
Mwanza. “Saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, nilipokea simu nikaelezwa mdogo wako ana shida. Nikakodi pikipiki, nilipofika kwa bibi nikabaini ameunguzwa kwa moto.” Ndivyo anavyoanza simulizi Joseph Semando, mkazi wa Kijiji cha Idetemiha, Kata ya Usagara akisimulia tukio la mfanyakazi wa ndani kumwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto. Tukio hilo alilotendewa Grace Joseph (17)…