Mambo yanayowasibu wachimbaji wadogo migodini, ufumbuzi watajwa
Dar es Salaam. Licha ya kuwa uchimbaji wa madini ni moja ya shughuli zinazovutia watu wengi, hususan wachimbaji wadogo, bado kundi hilo linakabiliwa na changamoto nyingi zinazohatarisha usalama na afya zao. Miongoni mwa changamoto kubwa ni matumizi ya kemikali hatari kama zebaki, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia 71 ya shughuli za uchimbaji nchini zinahusisha…