
Rais Samia awatangulia wenzake INEC, atumia dakika 46 kurejesha fomu
Dodoma. Mgombea wa kiti cha urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameshaingia Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kurudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo. Rais Samia ameingia saa 1.50 asubuhi leo Jumatano Agosti 27, 2025 akiwa kwenye msafara wa magari machache tofauti na alivyoingia siku ya kuchukua fomu Agosti…