Waliodai kubadilishiwa mtoto, waendelea kususia mwili
Arusha. Zikiwa zimepita siku 26 tangu matokeo ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) yatolewe, yakionesha Neema Kilugala (26), mkazi wa Mtaa wa Ndarvoi, hakubadilishiwa mtoto kama alivyodai, familia yake imeendelea kususia mwili ikisema wameamua kumwachia Mungu suala hilo. Familia hiyo ilianza kususia mwili wa mtoto huyo tangu Aprili 3, 2025, siku ambayo majibu ya DNA yalitoka….