Samia aahidi neema kwa wakulima wa tumbaku
Uyui. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakulima wa tumbaku mkoani Tabora kulipwa madai yao ya fedha na kwamba Serikali iko kwenye mazungumzo na kampuni mbili zinazodaiwa. Samia amebainisha hayo leo Septemba 11, 2025, wakati wa mkutano wake wa kampeni katika Wilaya ya Uyui,…