Makamu mwenyekiti wa TLP Zanzibar afariki Dunia
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Zanzibar Hamad Mkadam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, wakati akipatiwa matibabu ya afya kwenye moja ya hospitali kisiwani Pemba. Mkadam amefariki ikiwa ni mwezi mmoja na siku nne umepita tangu achaguliwa kuendelea kuhudumu kwenye nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Februari 2,2025 jijini Dar es Salaam….