‘Mzimu’ wa mastaa kubeti unavyotikisa Ligi Kuu
Miaka 30 iliyopita, kulikuwa na staa mmoja wa soka la Colombia, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi huko kwao. Unajua ilikuwaje? Ni stori ya kuhuzunisha ya Andrés Escobar Saldarriaga (Gentleman), moja ya mastaa waliokumbwa na janga kubwa kuwahi kutokea kwenye soka. Staa huyo alikuwa beki wa timu ya taifa ya Colombia na klabu za Atletico Nacional,…