Neema arejea nchini na ubingwa wa Perm Marathon

Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Neema Msuadi amerejea nchini akitokea Russia alikokwenda kushiriki mbio za Perm Marathon. Mbio hizo zilifanyika Oktoba, mwaka huu, jijini Perm ambako Neema alimaliza wa kwanza kwa muda wa saa 2:38:15 na kuwa Mtanzania wa pili kuongoza mwaka huu baada ya Gabriel Geay kufanya hivyo mwezi Februari akishinda Daegu Marathon za…

Read More

Watu wenye ulemavu 2,000 nchini kunufaika na pikipiki za nishati ya umeme

Babati. Watu wenye ulemavu 2,000 nchini watanufaika na pikipiki zenye magurudumu matatu zinazotumia nishati ya umeme, zinazotolewa bila malipo na taasisi ya Mati Foundation ya mjini Babati, mkoani Manyara. Taasisi hiyo imeeleza mpango wake wa kutoa pikipiki hizo zaidi ya 2,000 kwa makundi ya watu maalumu ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika shughuli za utafutaji….

Read More

Sh1.08 trilioni kusaidia utekelezaji uchumi wa buluu

Dar es Salaam. Ili kuongeza mchango wa uchumi wa buluu katika pato la Taifa, Umoja wa Ulaya umetoa zaidi ya Sh1.08 trilioni kwa benki za biashara nchini ili zikopeshwe kwa makundi yaliyopo katika mnyororo wa thamani wa sekta hiyo. Fedha hizo, zilizotolewa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB), tayari zinatolewa kupitia benki za CRDB,…

Read More

Sababu Lissu kuomba muda zaidi, Mahakama yatoa kauli

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu ameiomba Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, impe muda apitie uamuzi wa kesi zilizowasilishwa na upande wa mashtaka walipojibu hoja za pingamizi lake alizowasilisha katika kesi ya jinai inayomkabili. ‎Katika kesi hiyo, Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume cha kifungu…

Read More

ACT-Wazalendo waita nyomi hukumu ya kesi ya Mpina kesho

Dodoma. Chama cha ACT-Wazalendo kimeita wanachama, wadau na wale wanaotajwa kuwa wapenzi wa demokrasia kujitokeza kwa wingi kesho katika Mahakama Kuu Masijala Kuu Dodoma ili kusikiliza hukumu ya mtiania wao wa urais, Luhaga Mpina. Kaimu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Mbarala Maharagande, amewaambia waandishi wa habari leo, Jumatano, Septemba 10, 2025, kuwa wanatarajia kuwa na umati…

Read More

Matumizi ya AI kwenye matibabu yawaibua wataalamu wa afya

Dar es Salaam. Matumizi chanya ya teknolojia ya Akili Unde (AI) katika utambuzi wa magonjwa na urahisishaji wa matibabu yameelezwa kuwa miongoni mwa afua muhimu zinazoweza kubadilisha taswira ya sekta ya afya barani Afrika. Kauli hiyo imetolewa na wataalamu wa afya waliohudhuria ufunguzi wa Maonesho ya 26 ya Africa 2025 MEDEXPO, yanayofanyika kuanzia leo, Septemba…

Read More