Polisi kata, wananchi waja na mbinu ya kukabili uhalifu
Mwanza. Wakazi wa Kata ya Mabatini jijini hapa, wakishirikiana na Polisi Kata, wameanzisha mpango wa kuwaepusha vijana na vitendo vya kihalifu kwa kuwapatia elimu na mafunzo ya ujasiriamali. Mpango huu pia unawalenga wajane, wastaafu, wanawake na wazee kwa lengo la kuwawezesha kupata vyanzo vya mapato. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumapili, Agosti 18,…