NIKWAMBIE MAMA: Ahadi zenu zisigeuzwe chachandu za kampeni
Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 zinazidi kupamba moto. Kila mgombea katika nafasi anayoipigania amekuwa akiongeza kasi inayoambatana na vionjo vipya kwenye ahadi zake. Kuna wanaoleta ucheshi, lakini wengi wao wamebeba mafurushi ya ahadi bila kujali utekelezekaji wake. Mgombea ataahidi lolote hata kabla hajajua nini mahitaji ya mahala husika, atajinadi kutokomeza changamoto hata kabla hajazisikia. Tumesikia…