Jela miaka 30 kwa kubaka, kumpa ujauzito mwanafunzi
Simiyu. Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Luth Jacobo (50), mkulima wa kijiji cha Mwanundi, kata ya Sengwa wilayani humo, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 15 (jina linahifadhiwa) na kumsababishia ujauzito. Hukumu hiyo ilisomwa leo Jumanne, Septemba 9, 2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi…