Kura iwe ya moto au baridi…
Enzi zile tulipokuwa shuleni tulikuwa tukichanganywa na malumbano ya hoja. Kwa ufundi mkubwa, waandaaji walitoa mada iliyokuwa na majibu sawa. Kilichokuwa kikisikilizwa si majibu, bali ni ufundi wa mwanafunzi kutetea hoja zake. Kwa mfano: “Maisha bora ni ya kijijini au mjini?” Aliyejibu ni ya mjini alikuwa sawa kwa utetezi kuwa mjini kuna miundombinu ya kisasa…