
WAZIRI KOMBO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA
Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefanya mazungumzo na Bw. Ando Naoki, Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) pembezoni mwa Mkutano wa Tisa wa TICAD uliofanyika jijini Yokohama. Mheshimiwa Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA…