
MACHINGA NA BODABODA DAR WAWAONYA CHADEMA
Umoja wa Waendeshaji Bajaji, Bodaboda na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam, umetangaza kutoshiriki maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopangwa kufanyika Aprili 24, 2025, kuelekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, inatarajiwa kusikilizwa. Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo nchini, Steven Lusinde, ametoa tamko…