DK.SAMIA AAHIDI SERIKALI KUONGEZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KISASA KATIKA UTOAJI HUDUMA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Mtwara. MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakwenda kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo akili unde ili kuimarisha ufanisi katika uzalishaji na utoaji huduma ikiwemo kwenye kilimo. Dk.Samia ameyasema hayo leo Septemba 25,2025 alipokuwa akihitimisha mkutano wa kampeni katika Mkoa wa Mtwara baada ya kufanya mikutano…