Pamba Jiji yamkomalia beki Azam FC
BAADA ya beki wa kati wa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, Abdallah Kheri ‘Sebo’, kukitumikia kikosi cha Pamba Jiji kwa mkopo wa miezi sita msimu wa 2024-25, mabosi wa timu hiyo wanafanya mazungumzo ya kumsajili moja kwa moja. Awali, uongozi wa Azam ulimtoa nyota huyo kwa mkopo kwenda Fountain Gate katika…
BDL Ngoma ngumu, Dar City ikishinda jiooni
NUSU fainali ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), imeanza na moto huku timu zilizoshinda zikifanya hivyo kwa mbinde kutokana na ushindani uliopo ambao umeyanfanya mashindano hayo mwaka huu kuwa ya aina yake. Tofauti na miaka michache ya karibuni iliyopita ambapo ligi hiyo haikuwa na ushindani mkali kutokana na kutokuwa na uwekezaji…
Haya hapa mazao sita yatakayonyanyua uchumi wa Tanga
Tanga. Watalaam wa kilimo na ushirika kutoka halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga wamebainisha mazao yatakayowasaidia wananchi hususan wakulima kuinua uchumi wao. Akizungumza kwenye kikao kilichojumuisha wataalamu wa kilimo, ushirika na wadau wengine kilichofanyika leo Septemba 12, 2025 wilayani Handeni mkoani Tanga, Ofisa kilimo Mkoa, George Mmbaga amesema lazima wakulima wasaidiwe ili kulima kilimo chenye…
Wataalamu wataja sababu za changamoto za afya ya akili kwa wanaume
Tanga. Wataalamu wa afya ya akili wameeleza sababu zinazowafanya wanaume kukumbwa na changamoto za afya ya akili, hali inayochangia baadhi yao kufikia hatua ya kujiua, wakiamini hiyo ndiyo njia pekee ya kupata unafuu. Sababu hizo zimetolewa leo, Jumatatu, Machi 2, 2026, wakati wa warsha ya afya ya akili kwa wanaume iliyowakutanisha wadau mbalimbali mkoani Tanga,…
TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa, wananchi waonywa
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya tahadhari na angalizo la mvua kubwa kwa mikoa kadhaa, ikisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari stahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana na hali ya hewa mbaya. Katika taarifa hiyo, TMA imetahadharisha kuwa Ijumaa ya Machi 20, 2026, kunatarajiwa kuwa na mvua kubwa…
Othman aahidi neema kwa watumishi Zanzibar
Zanzibar. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT–Wazalendo, Othman Masoud Othman ameahidi kuwa iwapo atachaguliwa kuunda Serikali, ataweka kima cha chini cha mshahara wa Sh1 milioni kwa watumishi wa umma. Othman, ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT–Wazalendo, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza morali na ufanisi wa kazi kwa watumishi, huku akisisitiza kuwa kipaumbele kitatolewa…
Waziri Mkuu Mwigulu Awasili Arusha Kuzindua Miradi ya Kilimo na Kuzungumza na Wananchi
Global Publishers March 6, 2026 0 Comments Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 6, 2026 amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja mkoani Arusha katika Wilaya za Karatu na Monduli. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu anategemea kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa skimu za umwagiliaji…
Beldina na miongo miwili ya kufufua matumaini ya waliokata tamaa
Dar es Salaam. Kwa zaidi ya miongo miwili, jina la Beldina Nyakeke limekuwa sehemu ya sauti ya jamii ya Mkoa wa Mara. Akiwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Beldina ameitumia kalamu si tu kuripoti matukio, bali kama daraja la matumaini kwa jamii. Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa makala hii,…
WANANCHI DODOMA WASHAURI TBA KUJENGA NYUMBA ZA KUPANGISHA KWA WATU BINAFSI
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika Kliniki maalum ya kutatua kero za wananchi iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma, wameshauri Wakala kuanza kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya kupangishwa kwa watu binafsi kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyumba za kupanga katika mkoa huo. Ushauri huo…