
Presha, sukari, moyo vilivyoondoa uhai wa mbunge wa kwanza Moshi
Moshi. Wakati mamia ya waombolezaji wakifurika kwenye maziko ya aliyekuwa mbunge wa kwanza wa CCM Moshi mjini, Mkoa wa Kilimanjaro, John Mwanga (78), familia imeeleza kuwa baba yao alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na kisukari. Mwanga ambaye alikuwa mbunge wa kwanza wa Moshi mjini mwaka 1990-1995 kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alifariki…