
Mjadala kutokomeza ukatili kijinsia kufanyika Zanzibar
Unguja. Zanzibar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa saba wa viongozi mbalimbali duaniani kuhusu miji na maeneo salama ya umma, mjadala mkuu ukilenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Maeneo mengine yatakayojadiliwa ni namna ya kuanzisha na kuendeleza miji inayotumia teknolojia ya kisasa, kukuza utalii, biashara na uchumi wa buluu. Akizungumza na waandishi wa…