LIVERPOOL YAJIONDOA KUMUWANIA LENY YORO

Liverpool wamejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kumnunua mlinzi wa Manchester United Leny Yoro, 18, kutoka Lille kwa sababu walihisi anavutiwa zaidi na klabu ya Real Madrid. (Mirror) Powered by; @acbtanzania_ @kobemotor @betpawatanzania @wearekerry #TetesizaSokaUlaya #KonceptTvUpdates

Read More

Namna majitaka yalivyogeuzwa fursa Zanzibar

Unguja. Miaka michache iliyopita, Wazanzibari walikumbwa na maradhi ya mlipuko kama kipindupindu kutokana na mazingira kutokuwa safi. Mwaka 2016 watu 45 walipoteza maisha na 3,000 waliugua kisiwani humo. Hata hivyo, tangu kipindi hicho hakujawahi kushuhudiwa kasi ya ugonjwa huo baada chanjo iliyotolewa na Wizara ya Afya, ikiwa ni msaada kutoka mradi wa Shirika la Umoja…

Read More

KKKT kufanya harambee ujenzi kituo cha kulea watoto wenye usonji, Rais Samia mgeni rasmi

Dar es Salaam.  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limetangaza kuanza ujenzi wa kituo kipya cha watoto wenye usonji katika eneo la Kitopeni Bagamoyo mkoani Pwani. Usonji, au Autism Spectrum Disorder (ASD) ni hali ya ukuaji wa ubongo inayojumuisha changamoto katika maeneo ya mwingiliano wa kijamii, mawasiliano na tabia zinazojirudia. Hali hii inahitaji uangalizi…

Read More

Viongozi wa masoko watajwa uuzaji vizimba

Dar es Salaam. Migogoro ya vizimba vya biashara kwenye masoko nchini ni suala linalojitokeza mara kwa mara. Kwa kiasi kikubwa migogoro hii huwaathiri wafanyabiashara, mamlaka za serikali za mitaa na maendeleo ya masoko kwa ujumla. Ufuatiliaji uliofanywa na Mwananchi katika baadhi ya masoko nchini, migogoro hiyo huchangiwa na utaratibu wa utoaji wa vizimba unaodaiwa kugubikwa…

Read More

Serikali yataja chanzo katikakatika umeme

Unguja. Wakati baadhi ya wananchi na wafanyabiashara kisiwani hapa wakilalamikia katikakatika ya umeme, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Shaib Hassan Kaduara, amesema inasababishwa na ongezeko la watumiaji na wawekezaji nchini. Hata hivyo, amesema Serikali inatarajia kuleta msongo mpya wa umeme wenye megawati 220 kutoka Tanzania Bara mapema mwaka huu. “Unaotumika sasa una megawati…

Read More

Mwili mwingine mmoja wa ajali ya coaster watambuliwa

Morogoro. Mwili mmoja wa marehemu wa ajali ya Coaster umetambuliwa na hivyo kufanya jumla ya miili 11 ya waliokufa katika ajali hiyo kutambuliwa huku miili minne ikiwa bado haijatambuliwa.  Akizungumza na Mwananchi mganga mkuu mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Daniel Nkungu amemtaja marehemu aliyetambuliwa leo kuwa ni Sauda Sozigwa (35).  Dk…

Read More