
CCM yalaani kiongozi wake kuuawa Iringa
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimelaani tukio la Katibu wake, Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Christina Kibiki kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Christina ameuawa usiku wa kuamkia leo Jumatano Novemba 13, 2024, Kijiji cha Njiapanda ya Tosa, wilayani Iringa alipokuwa akiishi. Baada ya kushambuliwa, alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Tosamaganga…