
Wamarekani hawajawa tayari kuongozwa na Rais mwanamke
Wapenzi wa safu hii, niko jijini Washington D.C, mji mkuu wa Marekani, pamoja na mambo mengine nimepata fursa ya kuushuhudia uchaguzi wa Marekani, nchi inayoitwa “The Biggest Democracy” kumaanisha kuwa ni demokrasia kubwa kwa sababu ilipata uhuru wake Julai 4, 1776. Wagombea wakuu ni Kamala Harris anayewakilisha chama cha Democrats ambaye pia ni Makamu wa…