
Wadau mkutano wa UNCDF waishauri Serikali kudhibiti ubora wa vifaa vya nishati safi
Mwandishi Wetu Wadau wa Nishati Safi ya kupikia nchini, wameitaka Serikali kutunga sera ili kuwabana wanaoingiza vifaa visivyo na ubora kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kupikia. Hayo yamesemwa Jumatano Desemba 4, 2024 katika hoteli ya Coral Beach wakati wa mkutano wa kujadili sera katika sekta nishati ulioandaliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF)…