
Kampeni za mwisho mwisho Afrika Kusini kabla ya uchaguzi – DW – 26.05.2024
Uchaguzi huo unatarajiwa kuleta mabadiliko muhimu nchini Afrika Kusini baada ya miongo mitatu. Maelfu ya wafuasi wa chama kinachotawala cha African National Congress, ANC waliovalia nguo za rangi ya chama chao ambayo ni nyeusi, kijani na manjano walikusanyika katika uwanja wa soka mjini Johannesburg siku ya Jumamosi, kusikiliza hotuba ya kiongozi wa chama chao…