
Biteko: Bora uitwe mshamba, lakini usimamie maadili
Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kuna umuhimu mkubwa kwa jamii, wakiwamo vijana, wazazi, wanafunzi na Serikali kwa ujumla, kusimamia maadili ya Kitanzania. Amesema ni bora mtu uitwe mshamba, lakini asimamie misingi na tabia zote njema zinazotambulika katika jamii na kuachana na maadili yasiyofaa. Biteko ameyasema hayo…