
Makundi haya ya wajawazito hatarini kujifungua watoto wenye matatizo ya moyo
Arusha. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Naiz Majani ametaja makundi manne ya wanawake wajawazito walio katika hatari ya kujifungua watoto wenye matatizo ya moyo. Dk Majani amesema kuwa wajawazito wenye matatizo ya moyo au waliowahi kuzaa mtoto mwenye tatizo la moyo, au mwanafamilia…