TCD inavyotoa fursa kwa Chadema, ACT kuunda ushirikiano Uchaguzi Mkuu 2025

Habari ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), si yenye kushtua, maana ni utaratibu wa vyama vyenye wabunge kupishana katika uongozi wa taasisi hiyo. Habari kuwa Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, ndiye amekuwa Makamu Mwenyekiti wa TCD, ndiyo inasogeza mjadala. Mwenyekiti Chadema, Mwenyekiti TCD, halafu Kiongozi wa…

Read More

FCC yakubali kuanzisha ofisi mpaka wa Sirari

Katika kupata uelewa wa pamoja kuhusu shughuli za ukaguzi mipakani, Bodi na Menejimenti ya Tume ya Ushindani (FCC) imetembelea Kituo cha ukaguzi wa pamoja (OSBP) kilichopo Sirari Wilayani Tarime Mkoani Mara. Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika Jumatatu Julai Mosi, 2024, Bw. William Erio, Mkurugenzi Mkuu wa FCC ambaye pia ndiye Mkaguzi Mkuu wa Alama za…

Read More

Gari la mbunge lataifishwa, wahamiaji haramu watupwa jela

Moshi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na Mahakama ya Wilaya ya Moshi, zimeamuru kutaifishwa magari mawili yaliyokamatwa yakiwasafirisha wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia, likiwamo linalodaiwa kumilikiwa na mbunge. Mbali na kutaifishwa kwa magari hayo kuwa mali ya Serikali ya Tanzania, mahakama zimewahukumu wahamiaji hao kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja au kutumikia kifungo cha…

Read More

Msigwa anavyoongeza joto ubunge CCM Iringa Mjini

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mbunge wa zamani wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa alipokelewa kama mwanachama mpya wa CCM baada ya kuamua kuachana na chama chake cha Chadema alichokitumikia kwa zaidi ya miaka 20. Kuhamia kwa Msigwa CCM, siyo tu kumenogesha siasa za vyama vingi, bali pia kumeongeza joto la kisiasa katika jimbo la Iringa…

Read More

KONA YA FYATU MFYATUZI: Yaani mkimbinafsisha Bi Mkubwa namfyutua mtu

Mtukufu Dk Rahis, msikivu, mwenye maono, ndoto, uthubutu, ukimya, nk, naomba nimshukuru Mwenyezi Mungu, rahis, du! A’udhu billahi min ash-shaytaan-ir-rajeem. Nimemsahau Mtume! Naona yule anashangaa. Kwani nazusha? Wangapi, sijui chawa, sijui kunguni, wakianza kuchonga wanafanya hivyo kwa maangamizi yao na mafyatu wao? Nasikia kila mara rahis akisifiwa kuwa na ‘maono’ tena yasiyooneka. Kupitia maono, naona…

Read More

Lembeli: Operesheni Tokomeza ilinipa presha, iking’oa mawaziri wanne wa JK

Moja ya operesheni za Serikali zilizofanyika nchini na kugubikwa na mauaji ya watu, dhuluma na ukatili kwa wananchi ni Operesheni Tokomeza, iliyolenga kukabiliana na ujangili kwenye hifadhi za Taifa uliokuwa umekithiri wakati huo. Operesheni hiyo ilianza Oktoba 2023 hadi Novemba 2014, baada ya Serikali kusitisha kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa…

Read More

Veta yadhihirisha uwezo wake kwa watu wasioona

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Watu wasioona sasa wanaweza kupata ujuzi katika fani ya ufundi alluminiam na nyingine zinazotolewa na vyuo vya Veta kutokana kuwapo kwa maarifa yanayowawezesha kujifunza kirahisi. Raphael Mwambalaswa (39) asiyeona ambaye anaonekana kwenye banda la Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)…

Read More